Jumanne, 27 Septemba 2016

KUEREKEA OKTOBA 1 JOSEPH OMOG AKOMALIA SUALA LA UFUNGAJI SIMBA, AONYESHA NAMNA YA KUMALIZA KAZI MAPEMA

Kocha Joseph Omog amekomalia suala la upotezaji wa nafasi ambalo limekuwa kubwa katika kikosi chake cha Simba. Simba imeweka kambi mjini Morogoro, ikifanya maandalizi dhidi ya mechi ya watani wake Yanga, Oktoba Mosi. Katika mazoezi yake, Omog amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kufunga ikiwezekana kwa asilimia 90 katika nafasi wanazozipata. Kwani kila wanapofika kwenye eneo la lango, amekuwa akisimamisha mpira na kuwasiistiza namna ya kuzitumia nafasi. Simba imekuwa ikipoteza mechi zake nyingi za kufunga kila inapokuwa inashambulia katika mechi mbalimbali za ligi inazocheza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni