pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 26 Septemba 2016
Wakala: wa Pogba afunguka Raiola, asema Ibrahimovic angenivunja miguu kama Pogba asingetua United!
Wakala Mino Raiola amesema kuwa Zlatan Ibrahimovic kwa utani alitishia kumvunja miguu yake kama angeruhusu Paul Pogba kutua klabu nyingine tofauti na Manchester United.
Raiola ambaye anawawakilisha wachezaji wote hao wawili, pamoja na Henrikh Mkhitaryan, alizidalalia dili zote hizo tatu za mastaa hao kutua United msimu huu-ikiwa dili la Pogba la Paundi 89 Milioni kuwa ndio kubwa zaidi.
“Zlatan alinambia, ‘Ukimpeleka Pogba klabu nyingine, ntakuvunja miguu yako’,” alisema Raiola
Wachezaji hao wawili wamempa kocha Jose Mourinho nafasi nyingi ndani ya uwanja, lakini ikiwa Zlatan tayari ameshatulia haraka kwenye timu na tayari ameshafunga magoli manne kwa Mashetani Wekundu hao, Pogba amehangaika kutulia tangu arudi kwenye klabu yake hiyo ya utotoni.
Hata hivyo, Mfaransa huyo alikuwa katika kiwango bora chenye thamani ya gharama yake, pale alipofunga kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester City, Jumamosi hii.
Kuelekea mechi hiyo, Raiola, aliweka wazi hisia zake zifahamike kwamba Mourinho hamchezeshi Pogba katika eneo analolipendelea zaidi, ambayo ni sehemu ya kiungo mshambuliaji wa kushoto.
“Pogba bado anatakiwa atafute eneo lake kwenye tmu,” aliongeza Raiola. “Sehemu ninayopendelea acheze ni kiungo mshambuliaji wa kushoto.
“Kwa nguvu, stamina na ubunifu alionao… Pogba hatakuwa wa mchezo katika sehemu hiyo. Lakini ni Mourinho anayeamua.”
Huku Rooney akisugua benchi katika mechi dhidi ya Leicester, na Pogba akicheza katika sehemu ya kiungo mshambuliaji, bado tunabaki kusubiri kama kiwango bora kilichooneshwa Jumamosi kitamfanya Mourinho aendelee na mfumo uleule mpaka msimu unaisha au la.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni