pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 26 Septemba 2016
Hazard Afunguka atoa ya moyoni baada ya kipigo kutoka kwa Arsenal
Eden Hazard amekiri Chelsea hawapawi kuwa na kisingizio chochote kufuatia kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa mahasimu wao wa jijini London Arsenal, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Emirates Jumapili ya wikiendi iliyopita.
Chelsea hawakuwa wamefungwa kwenye michezo minne ya awali chini ya Antonio Conte, lakini wakajikuta wakifungwa na Liverpool 2-1 kabla ya kupata aibu ya kipigo kingine kutoka kwa Arsenal.
Arsenal walifunga mabao matatu ndani ya dakika 40 za mwanzo, na kuwaacha Chelsea wakiwa hawana lolote la kufanya na sasa Hazard amewaasa wachezaji wenzake kutotafuta kisingizio badala yake wapambane kwenye michezo ijayo.
“Hakua cha kujitetea,” Hazard aliiambia tovuti rasmi ya klabu hiyo. “Halikuwa jambo jema. Tulipoteza mipira mingi kirahisi.
“Tulienda pale kushinda mchezo lakini tulifanya makosa mengi sana, ukiangalia kwenye goli la kwanza, la pili na wakati tukihananika kufuta makosa tukaruhusu goli lingine na kuwa nyuma kwa mabao 3-0.
“Kinachotakiwa kwa sasa ni kugakikisha kila wiki tunapambana kupata matokeo. Tulifanya hivyo mbele ya Leicester lakini tukashindwa dhidi ya Arsenal ambao walikuwa nyumbani.
“Walicheza vizuri sana. Tunahitaji kuimarika zaidi. Kwenye michezo mitatu iliyopita tulitakiwa kupata pointi tisa lakini tumepata moja tu. Inasikitisha sana.
“Tunahitaji kufanyia marekebisho makosa yetu yote kwenye michezo mikubwa mingine inayofuata.”
Jumamosi ya wikiendi hii Chelsea watakuwa na kibarua kingine watakapokwaana na Hull City.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni