pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Septemba 2016
Rekodi 6 zilizovunjwa baada ya Arsenal kuivuruga Chelsea
Magoli ya Sanchez, Walcott na Ozil yalitosha kuwalaza mapema Chelsea kutokana na huzuni kubwa iliyokuwa imetawala mioyo yao kwani ni muda mrefu hawakuwa wameonja machungu ya kipigo kutoka kwa wapinzani wao wa mji mmoja.
Ukiachana na matokeo ya ushindi waliyopata Arsenal dhidi ya Chelsea, kuna rekodi kadhaa zimevunjwa katika mchezo huo. Hizi ni rekodi sita ambazo zimepigwa chini baada ya kushuhudia vijana wa Antonio Conte wakisulubiwa na wale wa mzee Wenger kwenye uwanja wa Emirates.
Antonio Conte alikuwa hajapoteza mechi kwa kipigo cha magoli 3-0 tangu October 2010, akiwa kocha wa Siena alichezea kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya Empoli.
Chelsea wamejikuta wakiwa nyuma kwa magoli matu katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Premier League kwa mara ya kwanza tangu May 2012 dhidi ya Liverpool (mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kushinda bao 4-1).
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza tangu October 2012 v Manchester United ambapo The Blues iliruhusu magoli mawili ndani ya dakika 15 za mwanzo kwenye mchezo wa Premier League.
Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa Arsene Wenger kwenye ligi dhidi ya Chelsea tangu Octber 2011 (alitoka sare mechi tatu na kupoteza mechi sita).
Hector Bellerin amekuwa beki aliyetoa assists nyingi zaidi ya mchezaji kwenye ligi ya England tangu kuanza kwa msimu uliopita (assists sita).
Theo Walcott amefunga mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu May 2013 (mechi tatu mfululizo za The Gunners).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni