Jumatano, 28 Septemba 2016

KOCHA WA YANGA AFUNGUKA HII NDIYO KAULI YA PLUIJM KUHUSIANA NA YANGA VS SIMBA

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema kuwa, mchezo wao na Simba utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji kushinda siku ya Jumamosi. Yanga walipoteza mchezo uliopita baada ya kufungwa bao 1-0 na Stand United ya mkoani Shinyanga na hivyo watakuwa na hasira kwenye mchezo huo wa Jumamosi kutokana na Simba wao kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji wikiendi iliyopita. Pluijm amesema, mtazamo wake wote kwa sasa ni kwenye mechi ya watani wa jadi kwa kuona ni jinsi gani timu yake inaweza kufanya vizuri huku akieleza kuwa anahitaji kuweka presha kubwa katika mchezo huo kwa kuwa anaamini kikosi chake kipo vizuri, ingawa mechi ijayo itakuwa ngumu sana. “Bila ya kutarajia tumepoteza mchezo wetu wa kwanza nje ya nyumbani dhidi ya Stand United, nimesikitishwa na matokeo kwa kuwa tulijiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tuliuanza vizuri mchezo. “Stand walicheza kwa mtindo wa kuzuia ambapo wachezaji wao tisa wote waliwaweka nyuma hivyo kufanya washambuliaji wangu kuwa katika wakati mgumu wa kuweza kufunga ikiwa ni pamoja na ubovu wa kiwanja pia ulichangia kufanya mchezo kuwa mgumu. “Tulitengeneza nafasi tatu katika kipindi cha kwanza na vilevile katika kipindi cha pili tulipata nafasi kama hizo lakini hatukufanikiwa kupata nafasi ya kufunga na iwapo tungefunga katika kipindi cha kwanza ingetusaidia, Stand walipata nafasi mbili katika kipindi cha pili na walifanikiwa kufunga bao moja kutokana na makosa yaliyofanywa na safu yangu ya ulinzi , lakini huo ndiyo mpira. “Mpira siku zote ni mchezo wa makosa na timu itakayofanya makosa machache ndiyo inayoshinda lakini kwa sasa naangalia mechi dhidi ya Simba ambayo ni mchezo mwingine utakaokuwa mgumu unaokutanisha timu mbili ambazo zote zinahitaji kushinda. “Nimekiandaa vizuri kikosi changu kuelekea mchezo huo, sihitaji kuweka presha kubwa kwa wachezaji wangu kueleka mchezo huo naamini tutafanya vizuri lakini wote kwa ujumla wapo fiti,” alisema Pluijm.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni