Jumapili, 25 Septemba 2016

Kocha wa Stand United Liewig afichua Behind the scene ushindi wa Stand United dhidi ya Yanga

Behind the scene kuna mambo mengi sana ambayo watu wanakosa kuyajua kwasababu yanaondolewa ili kinachomfikia mtazamaji kiwe ni bora licha ya kutumia nguvu nyingi kuyaficha makosa hayo. Nyuma ya ushindi wa Stand United 1-0 Yanga, haikuwa kitu rahisi kwa wachezaji wa timu hii ya wapigadebe wa Shinyanga mjini. shaffihdauda.co.tz ilikita kambi yake mjini Shinyanga kwa ajili ya kufatilia game kati ya wenyeji Stand United dhidi ya bingwa mtetezi wa VPL Yanga SC mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage . baada ya mechi kumalizika, ilibidi nimtafute kocha mkuu wa Stand United kibabu Patrick Liewig na kuzungumza nae ili aniambie nini siri ya ushindi wa timu yake mbele ya Yanga ambayo ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja wala kuruhusu goli kabla ya kukabiliana nayo. Kibabu akaanza kutiririka kwamba: “Sikua najali kuhusu Yanga badala yake nilikuwa naangalia timu yangu, vijana wangu walicheza kama mechi nyingine tu lakini kulikuwa na umakini mkubwa hasa katika eneo la ulinzi walicheza vizuri sana.” “Wachezaji walijituma na huenda tungefunga hata magoli zaidi lakini tulipoteza nafasi kadhaa, Yanga hawakupata nafasi ya yoyote ya kufunga.” Majibu ya kibabu yakanifanya nipenye swali dume kuhusu mwenendo wa timu hasa baada ya wadhamini wa timu hiyo kutangaza kukaa kando kutokana na mgogoro wa kiuongozi unaoitafuna klabu hiyo. “Timu hii inaweza ikafanya makubwa zaidi endapo uongozi utatekeleza wajibu wake, wiki hii ilikuwa ni ngumu kwa wachezaji kwasababu walikuwa wanadai haki zao kabla ya mechi hii lakini wananiheshimu na mimi nawaheshimu pia, ndio maana tumeshirikiana kupata matokeo haya. “Uongozi unatakiwa kuwawekea mazingira mazuri wachezaji kwa kuwatimizia stahiki zao”, hapa mzee Liewig alikuwa anamaanisha tayari wachezaji wameshaanza kuidai klabu ikiwa ni mechi sita tu hadi sasa zilizochezwa tangu kuanza kwa msimu mpya. “Wachezaji hawana jezi za kufanyia mazoezi. Tunatumia jezi za kuchezea mechi kwa ajili ya mazoezi, timu inamipira 15 pekee kwa ajili ya kufanyia mazoezi.” Wakati Liewig akiendelea kunipenyezea habari zaidi, ghafla alitokea kiongozi wa Stand na kuanza kumzuia kibabu asizungumze lakini kocha huyo wa zamani wa klabu ya Simba, aliendelea kusisitiza anachokisema ni kweli tupu. Hiyo inamaanisha kwamba, hali za wachezaji kiuchumi sio nzuri lakini waliamua kuipambania timu yao ili ipate matokeo labda huenda viongozi wakafanya kila liwezekanalo ili wawakamilishie mahitaji yao tofauti na kama wangepoteza mechi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni