Alhamisi, 22 Septemba 2016

Seluk azidi kumuandama Guardiola, sasa amemwambia muoga

Vita ya maneno kati ya wakala wa Yaya Toure Dimitri Seluk na kocha wa Manchester City Pep Guardiola imezidi kushika kasi baada ya Seluk kusema kuwa kocha huyo muoga. Seluk amesema kwamba kama kweli Guardiola ni kocha bora basi akafundishe timu kama Sunderland. Akiongea na kituo cha runinga cha Sky Sports, Seluk amesema: “Pep amepata mafanikio kwenye klabu za Barcelona na Bayern Munich, lakini angalia nyuma ya mafanikio yake kuna nini. “Kunzia alivyokuwa Barca, alikuta tayari timu imejengwa na Frank Rijkaard bado akawa na bahati nyingine ya kuwa na Lionel Messi. Ni Messi ndiye aliyeifanya Barca iwe juu na sio Pep. Luis Enrique ameonesha kwamba mafanikio ya Barca hayajajengwa na Guardiola. “Kama Pep anataka kuthibitisha kwamba yeye ni meneja bora, basi aende Real Zaragoza au Sunderland. Hapo ndipo tutathibitisha lakini tabia ya kwenda kwenye timu kubwa na kupata mafanikio halafu anasema yeye bora…hapana.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni