pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 28 Septemba 2016
Kocha wa Chelsea Antonio Conte, mguu upande mguu sawa
Gascoigne Brian
Bado naisubiri kuiona movie yake wapi itakapoishia, maana movie yake imeanza kunoga hata katikati haijafika. Mmoja kati ya wanadamu wanaoamini ulinzi kuliko unyumbulifu wa Hazard, ataamini vurugu za Zuma kule nyuma kuliko ubunifu wa Fabregas. Wakati mwingine udhaifu wa mwanadamu unatokana na kile anachokiamini yeye mwenyewe. Anahitaji sana utulivu wa Terry pale nyuma ili aweze kurudi katika hali ya kimchezo, ila Conte kumbuka maneno ya mwigizaji wa kiingereza mwanamama Audrey Hepburn aliposema NOTHING IS IMPOSSIBLE THE WORD ITS ELF (HAKUNA KITU KIGUMU KAMA NENO LENYEWE).
Ulimsikia Conte alichokiongea baada ya kipigo dhidi ya Arsenal? Alisema wachezaji wa Chelsea ni wa makaratasi akiwa na maana ya kuwa wachezaji wake unaweza kuwaogopa wakiwa katika orodha ila si uwezo wakiwa ndani ya uwanja. Naomba uyakumbuke maneno ya Audrey Hepburn. Yule Kante na Matic lazima ukubali kumfunga mmoja mnyororo ili uwiano katika kikosi uwepo. Yule Cahill taratibu anaanza kupoteza kujiamini ndio maana kila wakati anakuwa na makosa mengi pale nyuma.
Hesabu hazidanganyi na muda ni wakati nasubiri kuona ujio wa zuma na Terry pale nyuma tuone kitu gani kitatokea pale nyuma naona muunganiko wa Cahill na D.Luiz pale nyuma bado aujawa vizuri. Conte hakikisha miguu yako unaiweka sawa ili uweze kuwa katika mikono salama. Yule Abramovich mmoja kati ya wanadamu wachache sana wanaothamini ubora ulionao kuliko kusubiri utimilifu wako Conte njia pekee ya wewe kukaa salama katika mikono ya Abramovich ni kumpa furaha katika kikosi chako.
Yule Kante taratibu ameanza kuchoka sijui kwasababu ya kutumika sana msimu ulioisha, najaribu kuwaza hata sijapata jibu lililo hai dhidi yake.Yule Matic sio wa misimu miwili nyuma ameanza kuchoka kuanzia mwili mpaka miguu yake pia imeonyesha kuanza kuchoka naisubiri sana kuiona hii movie ya Conte dhidi ya wachezaji wake.
Nafasi ya yeye pekee kuweza kubaki ubora wake ni kuamua kubadilika kutoka kwenye ugumu na kuja kwenye kunyumbulika ndio sehemu ambayo Abrahimovich anaiwaza kila siku kuona Chelsea ikicheza soka la kuvutia. Ivanovic nilianza kukusahau kuelezea mapungufu yako wewe ndio matatizo zaidi kule nyuma. Conte akiamua kufumba macho na kufumbua jicho la ziada wewe ndio mtu wa kwanza kuondoka katika kikosi mmoja kati ya mchezaji unaekosa usawa dhidi ya wachezaji waliopo pale darajani.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni