Kikosi cha Yanga chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Hans van der Pluijm kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga tayari kupambana na Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Wachezaji wote waliosafiri na timu wamefanya mazoezi na hiyo inaashiria kikosi kizima kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Wakali wa Shinyanga mjini. Yanga imecheza mechi 5 imefunga magoli 8 huku ikiwa bado haijafungwa goli hata moja. Kwa upande wa Stand United nao hawajapoteza mchezo katika michezo yao mitano iliyopita. wamepata sare tatu na kushinda mechi mbili. Mechi zote walizoshinda ni zile walizocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mechi ya mwisho Yanga wameshinda 2-0 dhidi ya Mwadui FC ambao ni wapinzani wakubwa wa Stand United. Stand United nao walishinda 2-1 mchezo wao wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni