Jumapili, 25 Septemba 2016

Sakata la Toure limemgusa baba yake, atoa neno kwa Guardiola

Baba yake Yaya Toure amemuomba Pep Guardiola kumpa nafasi mwanawe aendelee kuitumikia Manchester City msimu huu. Toure amekosa nafasi mbele ya Guardiola baada ya wakala wake Dimitri Seluk kuwa katika mgongano na Guardiola. Tangu ujio wa Guardiola, Toure ameshacheza mchezo mmoja tu ambao ni wa mtoano wa Champions League dhidi ya Steaua Bucharest. Wakati wananingia kwenye mchezo huo, City tayari walikuwa ha hazina ya mabao 5-0 na tangu hapo, Toure hajawahi kucheza tena. Baba yake Toure ameiambia gazeti la The Sun: ‘Nina wasiwasi naye sana. Ni tatizo kubwa. Tunamuomba Guardiola arudi chini ili kijana aweze kupata nafasi tena. ‘Yeye ni bosi. Namuombea radhi kijana wangu, na amruhusu atimize majukumu yake.’ Toure ,33, amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake na klabu hiyo. Baba yake Toure ameongeza:Yaya anaipenda klabu yake sana, ni mchezaji muhimu kwenye timu, ana morali kubwa ya kuendelea kucheza. “Mimi kama mzazi ninaweza pia kumzungumzia, naamini ataendelea kubaki pale. Na atafanya uamuzi sasa kutokana na hali inayomkabili.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni