pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Septemba 2016
AZAM FC 'YAUWAWA' MTWARA, MBEYA CITY YACHAPWA, MTIBWA IKIAMBULIA SARE NYUMBANI
Azam FC imepoteza mechi yake ya pili leo baada ya kuchapwa kwa mabao 2-1 na wenyeji wake Ndanda FC.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Azam FC ilipoteza mechi hiyo katika dakika za mwisho baada ya kucheza vizuri katika kipindi chote cha kwanza.
Nafasi kadhaa walizopoteza, pia katika kipindi cha pili watazijutia kwa kuwa Ndanda walitumia vizuri nafasi walizozipata.
Nao JKT Ruvu, wamezidi kuonyesha hawataki tani baada ya kuitwanga Mbeya City kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa mkoani Pwani.
Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani, baada ya kuongoza kwa muda mrefu imejikuta ikizuiliwa na kukamtwa kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbao FC.
Mtibwa Sugar waliongoza kwa muda mrefu, jioooni wakaruhusu bao hilo la kusawazisha na kuwafanya wapoteze pointi nyingine mbili.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni