Jumamosi, 24 Septemba 2016

Barcelona bila ya Messi yafanya kufuru ya magoli ugenini La Liga

Barcelona wamejitahidi kujikwamua licha kukosekana kwa Lionel Messi na kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Sporting Gijon huku magoli matati ya mwsh yakifungwa dakika tisa za mwisho. Luis Suarez alifunga bao la kwanza kabla ya Rafinha kuongeza la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0 mpaka mapumziko. Nahodha wa Sporting Gijon Alberto Lora alitolewa nje dakika ya 74, kuongeza mengine mawili na Arda Turan kufunga moja na kufanya idadi ya magoli 5-0. Lora alikuwa ana kadi ya njano wakati alipokuwa ameoneshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumfanyia faulo Sergi Roberto, ambaye alijibu kwa kutengeneza pasi ya goli la tatu na la nne, wakati huo akiwa tayari ametoa pasi ya goli la Rafinha. Paco Alcacer, bado anapambana khakikisha anaifunga goli lake la kwanza akiwa Barca kufuatia usajili wake kutoka Valencia. Turan alifunga bao la nne kwa krosi nzuri kutoka winga ya kulia, kabla ya Neymar kufunga mahesabu baada ya kuitendea haki pasi ya Denis Suarez alyekuwa ameingia kutokea benchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni