Jumatano, 21 Septemba 2016

LYANGA MAMBO SAFI OMAN, AFUZU MAJARIBIO NA KUPEA MKATABA WAKE MKONONI

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Danny Lyanga amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Fanja FC ya Oman. Lyanga alifuzu majaribio tokea wiki iliyopita lakini rasmi jana amekabidhiwa mkataba wake. Simba iliamua kumuachia aende Oman baada ya usajili wake mpya wa washambuliaji kama Laudit Mavugo, Fredric Blagnon na viungo kama Shiza Kichuya na Mohammed Ibrahim.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni