Jumamosi, 24 Septemba 2016

Manara Afunguka Asema Ushindi wa Simba vs Majimaji, atangaza kaulimbiu ya Simba kuelekea October 1

Waswahili husema kipato huleta majivuno, ushindi wa 4-0 ilioupata Simba dhidi ya Majimaji FC, umemfanya msemaji wa klabu hiyo Haji Manara atangaze kauli mbiu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ kwa msimu huu. Manara amesema msimu huu Simba haidharau timu timu yeyote kwenye ligi huku akisisitiza timu yake imejipanga kuongoza ligi kudumu hadi mwisho. “Macho yetu na masikio yetu tunaelekeza October 1, ni mechi ya kawaida kama mechi nyingine ya ligi na hatuipi u-special wowote ule. U-special wake ni kwasababu ya kucharuana kwa mashabiki lakini uzito ni ulele tulioutoa kwenye mechi ya Majimaji ndio tutautoa ligi nzima hatutadharau timu yeyote”, amesema Manara mara baada ya mechi kati ya Simba dhidi ya Majimaji. “Tutacheza na Yanga kama tunacheza na mkubwa mwenzetu, hatujali hii ni timu ndogo au kubwa tunatakiwa tuongoze ligi kwa kudumu hadi ligi inamalizika.” “Hatutadharau mechi inayokuja, mechi ya leo ni sawa na mechi inayokuja bila kujali ni Yanga au timu nyingine yeyeyote, kila mechi ni fainali hiyo ndiyo kaulimbiu ya Simba msimu huu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni