Jumamosi, 24 Septemba 2016

Liverpool yafanya mauaji Anfield Yaichapa Hull City 5-1

Liverpool wameshinda kwa kishindo baada ya kuwafunga Hull City mabao 5-1, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Anfield. Magoli ya Liverpool yamefungwa na Adam Lallana dakika ya 17, James Milne dakika ya 30, Sadio Mane dakika ya 36, Philippe Coutinho dakika ya 52 na James Milner tena dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati. Bao pekee wa Hull City limefungwa na David Meyler Mchezaji wa Hull City Ahmed El Mohamady alipewa kadi nyekundu baada ya kushika mpira ndani ya eneo la hatari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni