Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya taiga ya England, Gareth Southgate ndiye anachukua jukumu la kuinoa timu hiyo. Southgate, anachukua nafasi huyo baada ya Sam Allardyce kuamua kuachia ngazi katakana na kashfa iliyomkumba. Allardyce maarufu kama Big Sam amedumu kwa sikh 61 baada ya kupata mkataba mnono wa kuinoa England. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye mtego na kurekodiwa akipiga dili ya upindishaji wa sheria za FA. Southgate ambaye aliwahi kufanya mahojiano na Salehjembe, wakati akiwa kocha wa Middelesbrough, ataanza kuiongoza England katika mechi yake dhidi ya Malta Oktoba 8. Imeelezwa kocha huyo ataingoza England kwa mechi nne kabla ya uamuzi wa suala la kocha mpya kupitishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni