Alhamisi, 22 Septemba 2016

Barcelona Majanga yapata pigo, kumkosa Messi wiki tatu

Staa wa Barcelona Lionel Messi atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu baada ya kupata maumivu ya nyonga kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa Nou Camp na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 jana. Nohodha huyo wa Argentina alipata maumivu hayo punde tu baada ya kumaliza kuwania mpira na beki wa Atletico Madrid Diego Godin na kuanza kuashiria hali ya maumivu hasa kwenye upande wake wa kulia.  Jeraha hilo la Messi inaelezwa awali alipata wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina wiki chache zilizopita, na staa huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa Champions League dhidi ya Borussia Monchengladbach. Messi pia atakosa michezo La Liga dhidi ya timu za Sporting Gijon na Celta Vigo, na atakuwa hatihati pia kucheza mchezo wa Champions League dhidi ya Manchester City utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba. “Kumkosa Messi maana yake ni pigo katika soka. Tunapokuwa na Messi maana yake tuko imara, lakini tutajitahidi kuwa imara hata bila ya uwepo wake,” kocha wa Barcelona Luis Enrique aliwaambia waandishi baada ya mchezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni