pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Septemba 2016
MATCH PREVIEW; ARSENAL KULIPA KISASI LEO DHIDI YA CHELSEA...
Arsenal leo wako nyumbani wakiwa na mtihani mzito watakapokuwa wakiwakaribisha mahasimu wao wa jiji la London Chelsea katika mchezo wa EPL utakaofanyika kunako Uwanja wa Emirates saa 1:30 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.
Arsenal wanaingia katika mchezo huu wakiwa na imani kubwa kutokana na kuwa na kikosi imara msimu kunzia upande wa safu ya ulinzi mpaka ushambuliaji ukilinganisha na misimu kadhaa iliyopita.
Taarifa muhimu kwa kila timu
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud leo anaweza kurejea baada ya kukosekana katika michezo miwli iliyopita kutokana na kusmbuliwa na majeraha.
Hata hivyo kiungo Aaron Ramsey bado ataendelea kuwa nje akiunguza jeraha lake la misuli ya paja na kukadiriwa kurudi takriban wiki tatu zijazo.
Kwa upande wa Chelsea, nahodha wao John Terry ataendelea kukosa mchezo wa leo ambao ni mchezo wa tatu mfululizo kufuatia kuendelea na tiba ya jeraha lake la mguu.
Beki mwenzake Mfaransa Kurt Zouma bado ataendelea kubaki nje licha kuwa tayari ameanza mazoezi madogo-madogo.
Kauli za makocha wa timu zote mbili
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger juu ya nidhamu kwa timu yake: “Tumeongea kuhusu hilo kwasababu katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Chelsea tumecheza tukiwa pungufu.”
“Hivyo mchezo wa leo utakuwa muhimu sana kwetu kupata matokeo, lakini muhimu zaidi kucheza kwa nidhamu kubwa.”
Kocha wa Chelsea Antonio Conte: “Huu ni mchezo mkubwa sana unawakutanisha mahasimu wakubwa. Ni muhimu zaidi kucheza soka safi.
“Zaidi ya hapo baada ya kufungwa na Liverpool kulitufedhehesha. Lakini leo itabidi tupambane sana maana tunafahamu kuwa tunacheza na si tu timu kubwa bali mahasimu wakubwa.”
Dondoo muhimu za mchezo
Head-to-head
Chelsea hawajapoteza mechi tisa zilizopita za Premier League dhidi ya Arsenal (wameshinda mara sita, droo mara 3).
Chelsea hawajapoteza mchezo wowote kati ya mitano ya mwisho waliyocheza katika Uwanja wa Emirates (ushindi mara 2, droo mara 3) tangu mara ya mwisho walivyofungwa 3-1 Desemba 2010. Na wameruhusu goli moja tu katika michezo yote hiyo.
Arsenal wameshinda kupata goli mbele ya Chelsea kwenye mechi sita zilizopita.
Katika mechi tano za mwisho dhidi ya Chelsea, jumla ya wachezaji wanne wa Arsenal wamejikuta wakitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Arsenal
Arsenal wanajiandaa kupata ushindi wao wa nne mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu Oktoba mwaka 2015 walivyoweka rekodi ya kushinda mechi tano mfululizo.
Arsenal wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 15 iliyopita (wameshinda mara 8, droo mara nne).
Alexis Sanchez ameshindwa kufunga hata goli moja kwenye michezo minne ya ligi akiwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Chelsea
Kocha wa Chelsea Antonio Conte anaweza kucheza michezo mitatu bila ya ushindi kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho walivyopata sare nne mfululizo wakati akiwa Juventus Macih 2012.
Conte hajawahi kupoteza michezo ya ligi mfululizo tangu Desemba 2009 wakati akiwa Atlanta.
Chelsea wamepata clean sheet moja tu kwenye michezo yao ya ligi 12 iliyopita, huku wakiruhusu bao kwenye kila mchezo kati ya michezo sita iliyopita ya ugenini.
Diego Costa amefunga magoli matano kwenye michezo mitano ya Premier League msimu huu, akifunga kwenye kila mchezo kati ya mitatu iliyopita.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni