Kituo cha Runinga kinachozidi kufanya vema kwa kasi chaAzam TV, jana Jumnne kimezundua promosheni yake mpya ya Full Dowzii Kutwa Mara Tatu ambayo itakuwa mahususi kwa ajili ya wateja wao wapya. Katika promosheni hiyo, mteja atapewa king’amuzi, dishi, rimoti na vifaa vyake vyote pamoja na kuunganishiwa king’amuzi hicho endapo mteja huyo atalipia kifurushi kikubwa cha Azam Play kwa mwaka mmoja. Mkurugenzi wa Matukio wa Azam TV, Yahya Mohamed, amesema: “kwa kawaida mteja mpya hununua king’amuzi cha Azam TV pamoja na vifaa vyake vyote kwa Sh 135,000, huku gharama za ufundi zikiwa ni Sh 30,000 ambapo jumla ni Sh 165,000. “Lakini mteja mpya ukilipia Sh 336,000 kwa ajili ya kifurushi cha Azam Play kwa mwaka, utaokoa Sh 165,000. Hivyo niwaambie tu wateja wetu Azam tumekuja kwa ajili ya kuwakomboa na kupata burudani kila siku bila ya kikomo.” Aidha, Mohamed alisema, Azam TV ina vifurushi vitatu vya mwezi ambavyo ni Azam Pure Sh 15,000, Azam Plus Sh 23,000 na Azam Play Sh 28,000 ambapo kifurushi hicho kikubwa ndicho kinachohusishwa na promosheni hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni