pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 25 Septemba 2016
Sikia hii Kijembe cha Zitto Kabwe kwa Yanga baada ya kufungwa na Stand United
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Simba, ame-tweet kwenye account yake ya twitter akiipiga kijembe klabu ya Yanga baada ya kufungwa goli 1-0 na Stand United mkoani Shinyanga.
Zitto amewaambia Yanga kwamba, waliweka umakini mkubwa kwenye mechi kati ya Wabunge wa Yanga dhidi ya Wabunge wa Simba huku wakisahau mechi yao muhimu ya Shinyanga dhidi ya Stand United.
Mwanasiasa huyo maarufu nchini aliendelea kuwatania mashabiki wa Yanga kwa kuandika kuwa mechi kati ya Stand United dhidi ya Yanga imeahirishwa hivyo watu wapuuze taarifa za matokeo ya Yanga kufungwa na Stand kwani taarifa za timu yao kufungwa na Stand United hazina ukweli wowote.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni