Jumamosi, 24 Septemba 2016

LIVE KUTOKA TAIFA: SIMBA 1 VS MAJIMAJI 0 (MAPUMZIKO)

MAPUMZIKO -Mwamuzi Rudovick Charles kapuliza kipenga kuashiria ni mapumziko -Kipa wa Amani Simba, yuko chini akipatiwa matibabu DAKIKA 2 ZA NYONGEZA Dk 44, Mavugo anawalamba chenga mabeki wa Majimaji lakini shuti lake linakuwa mtoto kabisa Dk 38 hadi 42, mpira unaonekana umepunguza kasi kwa kiasi kikubwa kabisa Dk 36, krosi safi ya Mohamed Zimbwe, inamkuta Mzamiru anapiga vizuri kabisa lakini hakulenga lango Dk 34, Mavugo anaingia vizuri kabisa katika eneo la hatari, lakini anajaribu kufunga katika eneo ambalo angeweza kutoa pasi Dk 33, Kichuya anaukwamisha mpira wavuni, lakini mwamuzi msaidizi, Mugando anasema alikuwa ameishaotea Dk 32, nafasi nzuri kabisa ya kwanza ya Majimaji, George Mpole akiwa amebaki na kipa wa Simba, anashindwa kulenga lango Dk 31, Kichuya anapiga shuti la mpindo, lakini Amani Simba anakuwa makini na kuokoa kwa umakini kabisa SUB Dk 25, Ndemla anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu Dk 24, Kichuya anapoteza nafasi nzuri baada ya kupaisha shuti juu karibu na lango la Majimaji Dk 22, Ajib anakwenda nje baada ya kuumia, inaonekana nafasi yake itachukuliwa na Said Ndemla Dk 21 mpira unasimama, Ajib yuko chini akipatiwa matibabu Dk 19, Simba wanafanya shambulizi tena, Mnyate anaingia vizuri kabisa lakini mabeki wanaokoa vizuri kabisa Dk 14 hadi 16, Simba, Majimaji pia wanagongeana mpira katikati ya uwanja zaidi Dk 13, Ajibu anamtoka Hamad Kipobile na kupiga shuti la chinichini lakini linatoka sentimeta chache nje ya lango la Majimaji, Amani Simba anawalaumu mabeki wake hapa Dk 12 krosi safi ya Mnyate lakini inakosa mtu, Majimaji wanachukua na kuanza kugongeana lakini wanatuliza mpira kwa kucheza taratibu Dk 10, shambulizi la kwanza la Majimaji lakini Mollel anachelewa kuuwahi mpiga na kipa Vicent wa Simba anawahi na kudaka Dk 8 hadi 9, Simba wanaonekana kushusha presha na kugongeana taratibu Dk 7, Simba wanagongeana vizuri na kuingia hatari kabisa, lakini Lulanga Mapunda anaokoa na kuwa kona, Simba wanaichonga lakini haina matunda GOOOOOO Dk 4, Jamal Simba Mnyate anaipatia Simba bao la kwanza baada ya krosi safi ya Mavugo, Ajib akapiga shuti la chini lakini kwa ulaiiiniii Mnyate anamalizia baada ya kipa Amani Simba, kupangua Dk 2, Simba wanapaleka shambulizi jingine baada ya Majimaji kushambulia lakini bado linakuwa dhaifu Dk ya 1, mechi imeanza kwa kasi kubwa na Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji, lakini ni offside.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni