pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 22 Septemba 2016
BOCCO AWA MCHEZAJI BORA WA KWANZA LIGI KUU BARA MSIMU WA 2016-17
Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Agosti kwa msimu wa 2016/2017.
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Azam FC aliwashinda wachezaji Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu. Katika mechi mbili ilizocheza katika mwezi huo, Bocco aliifungia timu yake mabao matatu likiwemo la kusawazisha dhidi ya African Lyon.
Alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa kupata pointi nne kati ya sita.
Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni