Jumanne, 20 Septemba 2016

Chelsea, Liverpool, Arsenal zote leo vitani EFL Cup, ratiba yote ipo hapa

Michezo ya raundi ya tatu ya Kombe la Ligi, nchini England maarufu kama EFL CUP, ambalo awali lilikuwa likiitwa Capital One Cup, inatarajiwa kuchezwa leo na kesho Usiku. Kwa mara ya kwanza timu zote vigogo za EPL, zikiwemo zinazoshiriki Mashindano ya UEFA. Mabingwa Watetezi Manchester City wao kesho watakuwa ugenini kupambana na Swansea City. Mabingwa wa EPL, Leicester City leo watakuwa nyumbani katika Uwanja wa King Power kuwakaribisha Chelsea. Timu nyingine za EPL ambazo leo zitakuwa dimbani ni Liverpool na Arsenal ambazo zote zitakuwa ugenini kuzivaa timu za madaraja ya chini. Derby County watacheza na Liverpool na Nottingham Forest kuivaa Arsenal. Kesho Jumatano Man United wapo Ugenini kuivaa Timu ya Daraja la chini Northampton Town. Ratiba nzima hii hapa Jumanne

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni