Jumanne, 20 Septemba 2016

SCHUMACHER HAWEZI KUTEMBEA Mwanasheria wa dereva wa zamani Michael Schumacher, Felix Damm jana ameiambia mahakama huko nchini Ujerumani kuwa bingwa huyo wa zamani wa Formular 1 hawezi kabisa kutembea kufuatia ajali aliyoipata mwaka 2013. Schumacher,47, aliumia kichwani baada ya kupata ajali mwaka 2013 wakati akicheza mchezo wa kuteleza katika theluji katika milima mirefu ya huko nchini Ufaransa. Felix Damm ameongea hayo mahakamani kwa niaba ya familia ya Schumacher ambayo imefungua shitaka dhidi ya jarida la nchini ujerumani linaloitwa Bunte ambalo disemba mwaka jana liliandika kuwa dereva huyo Mjerumani sasa anaweza kutembea. Damm amesema kuwa bingwa huyo mara 7 wa Formular 1 hawezi kutembea mwenyewe na hata kwa msaada wa wataalamu Dereva huyo wa zamani wa timu za Ferrari,Mercedes baada ya kupata ajali mwaka 2013 aliwekwa katika sehemu ya matibabu maalum kwa miezi 6 kabla ya kupelekwa nyumbani kwake Switzerland kuendelea na matibabu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni