Jumatatu, 19 Septemba 2016

BAADA YA VIPIGO VITATU MOURINHO AANZA LAWAMA KWA WACHEZAJI WAKE

Jose Mourinho ametupa lawama zake Luke Shaw baada ya Manchester United kufungwa mchezo wa tatu mfululizo jana dhidi ya Watford. Mreno huyo pia alimtupia lawama mwamuzi Michael Oliver kwa kushindwa kutoa penati baada ya Miguel Britos kumfanyia faulo Anthony Martial kuelekea maandalizi ya goli la Etienne Capoue. Hii ni mara ya tatu anawalaumu marefa, mechi nyingine alizowalaumu marefa ni dhidi ya Manchester City, Feyenoord na hii ya Watford, mechi ambazo zote amepoteza. Malalamiko ya Mourinho kwa Shaw anaeleza sababu kwamba, beki huyo alishindwa kumdhibiti Nordin Amrabat kabla ya Juan Camilo Zuniga kufunga goli dakika ya 83. Mourinho aliongeza kuwa hali hiyo pia ilitokea kweye mchezo dhidi ya Manchester City pale Aleksandar Kolarov alipopiga mpira mrefu ulioshindwa kudhibitiwa kirahisi na mabeki wa Manchester United. Alisema: “Goli la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Man City na hili la pili dhidi ya Watford, unaweza kuona kuna ufanano mkubwa sana, kwa maana ya kwamba Kolarov amepata mpira akiwa na wakati mgumu kwenye kona, sasa wachezaji wangu badala ya kumfuata ili kumnyima nafasi wao wakampa nafasi. “Na hili goli la pili la Watford, Amrabat amepokea mpira na beki wetu namba tatu yuko umbali wa mita 25 badala ya kukaa umbali wa mita tano. Lakini hata kama upo umbali wa mita 25 unapaswa kwenda kuziba nafasi lakini wapi hakijafanyika hicho kitu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni