Mino Raiola ambaye ni wakala wa wachezaji wengi mastaa katika ligi tofauti, akiwemo Mario Balotelli ambaye sasa anaichezea Nice ya Ufaransa amesema kuwa anaamini ipo siku Balotelli atarejea kucheza katika Premier League. Balotelli ameshacheza katika Premier League ndani ya Manchester City na Liverpool lakini kote hakupata mafanikio makubwa. Raiola amenukuliwa akisema: "Ufaransa inamhitaji kama walivyokuwa wakimhitaji Zlatan (Ibrahimovic). Yupo vizuri lakini ipo siku atarejea Premier League." Balotelli alitua Nice baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na Kocha wa Liverpool, Klopp ambaye aliwekaza wazi kuwa hamuhitaji katika kikosi chake. "Mario na Jurgen Klopp hawakupata nafasi kwa kuwa Klopp hakutaka kumopa nafasi," alisema Raiola na kuongeza. "Klopp alikuwa akimuona Balotelli kama mpuuzi tu.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni