Jumatatu, 19 Septemba 2016

MASHABIKI WA ARSENAL SIKIA HAYA YA WAKALA WA POGBA MINO RAIOLA ARUSHA KIJEMBE KWA ARSENAL JUU YA POGBA

Wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amezungumzia uhamisho wa mchezaji wake kwenda Manchester United, na kudai kwamba ingekuwa rahisi pia kwenda Real Madrid, lakini akiondoa uwezekano wowote wa mchezaji huyo kwenda Arsenal kwa kusema timu hiyo haina soka la kuweza kuvutia usajili wa mchezaji wa kiwango cha dunia. Raiola amesisitiza kwamba ni kweli Arsenal wana pesa za kufanya usajili huo na kuonesha heshima yake waziwazi kwa Arsene Wenger, japokuwa anaamini timu hiyo imekosa kujiamini pale linapokuja suala la usajili wa wachezaji. “Hapa sizungumzii tu suala la matumizi ya pesa,” Raiola ameliambia gazeti la Daily Mail. “Ni suala la kufanya maamuzi na kusema ‘ndio huyu ni mchezaji wangu’. Arsenal wana pesa, lakini wana mpira wa kuvutia wachezaji? “Namheshimu sana Arsene Wenger. Ana falsafa ambazo anapenda kuzitumia ambapo hupenda kusema kiasi ninacholipa hakiendani na thamani ya mchezaji, lakini sio mbaya hakuna shida. Najua vizuri kwamba Wenger anampenda Pogba lakini bei ambayo Juventus waliiweka kumuuza mchezaji huyo haiendani na falsafa zake. “Kwa upande wa Real Madrid, Zidane alikuwa tayari kwa kila kitu lakini hatukuwa na uhakika kama klabu yake ilikuwa ina mtazamo kama wake. Manchester United walitutumia message na kusema: ‘hii ni klabu kubwa duniani, hakuna tunachoweza kushindwa’.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni