Jumanne, 23 Agosti 2016

WAARABU WALIOFUNGWA NA YANGA WASONGA MBELE KIMAZABE

Licha ya kufungwa na Yanga katika mchezo wa Agosti 13, timu ya Mo Bejaia ya Algeria ambayo pia imelingana pointi na Medeama ya Ghana, lakini kanuni za Kombe la Shirikisho zimeiwezesha timu hiyo ya Algeria kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali. Mo Bejaia imemaliza hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 8, sawa na Medeama lakini kwa kuwa katika mchezo wa leo Jumanne uliozikutanisha timu hizo kicha Mo Bejaia imeshinda kwa bao 1-0, imefanikiwa kusonga mbele kwa kuwa kanuni inasema mara baada ya timu kufungana pointi kinachoangaliwa ni ‘head to head’ pindi zilipokutana. Wadau wengi walijua kuwa baada ya kulingana pointi kitakachoangaliwa ni idadi ya mabao ya kufunga au tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga lakini kumbe sivyo.  Mo Bejaia Kwa kuwa zilipokutana awali, zilitosa suluhu ya 0-0, hivyo sasa Mo Bejaia imesonga mbele kwa kusaidiwa na ushindi huo wa pili ilioupata leo. TP Mazembe imeongoza kundi kwa kuwa na pointi 13, wakati Yanga imeshika mkia ikiwa na pointi nne. Yanga iliifunga Mo Bejaia bao 1-0 jijini Dar es Salaa wakati Mo Bejaia nayo iliifunga Yanga bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni