Jumatano, 24 Agosti 2016

EXCLUSIVE.....BARAGHASHIA YA MZEE AKILIMALI YAPATIKANA, ALIYEIIBA APATA KICHAPO

Baada ya jana kuripotiwa kuwa Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Mzee Akilimali aliibiwa kofia aina ya baraghashia, habari nzuri ni kuwa kofia hiyo imepatikana. Tukio hilo ambalo lilitokea juzi asubuhi wakati Mzee Akilimali alipokuwa Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam alipokwenda kumtembelea rafiki yake Mzee Mwika, limekuwa gumzo na kuonekana kama kichekesho. Kwenye  picha ya Nyumba ambayo ndipo tukio lililopotokea, kushoto ni Mzee Akilimali akiwa na wenyeji wake. Akizungumzia suala hilo Mzee Akilimali alikuwa na haya ya kusema: "Acha kabisa hawa vibaka wala unga siyo watu wazuri kabisa, aisee waliniibia kofia yangu ambayo huwa naivaa kila siku, lakini nashukuru imepatikana. "Kofia hiyo imepatikana licha ya kuwa tayari ilikuwa imeshauzwa na vijana wawili ambao walikuwa wameshaiuza. "Niliahidiwa kuwa lazima nitaipata kofia yangu kwa kuwa wenyeji wangu waliniambia wanajua sehemu ambapo wanauza vitu vya wizi. “Unajua mazungira ya kuniibia yalitokana na mimi kuiacha nilipokuwa nimekaa kwenda kununua mihogo kwa ajili ya kunywa chai, sasa wakati nanyanyuka naenda kununua ndiyo kibaka akamzidi maarifa Mzee Mwika na kuiiba. “Kijana mmoja aliyeiba amekamatwa na kupewa kipigo kikali kabla ya kufikishwa kituo cha Polisi Mtoni Mtongani.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni