Baada ya kuanza msimu vizuri kwa kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo za Premier League, wachezaji wa kikosi cha kwanza wa Manchester United walikuwa na mapumziko ya siku mbili, wamerejea mzigoni jana na kuanza mazoezi. Man United ambayo imezifunga Bournemouth na Southampton katika mechi hizo za kwanza inatarajajiwa kukutana na Hull City, wikiendi inayofuata. Katika mazoezi ya leo kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Carrington, mastaa wa timu hiyo walionekana wakiwa na furaha kabla na hata baada ya kuanza mazoezi chini ya Kocha Jose Mourinho. Baadhi ya mastaa hao ni Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Wayne Rooney ambao walionekana wakitaniana na kucheka. MECHI 5 ZIJAZO ZA UNITED KATIKA PREMIER NI: August 27: Hull (away) September 10: Man City (home) September 18: Watford (away) September 24: Leicester (home) October 2: Stoke (home)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni