Jumamosi, 14 Januari 2017

RAFIKI YAKE SAMATTA, ATUA LEICESTER NA KUANZA NA KIPIGO CHA CHELSEA Beki Mnigeria, Wilfred Ndidi ameianza Ligi Kuu England timu yake ya Leicester City inakutana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Chelsea. Ndidi ametokea Genk ya Ubelgiji ambayo alikuwa akicheza pamoja na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta. SAMATTA NA NDIDI Genk imekuwa ikisifika kwa kuuza wachezaji kwenye timu mbalimbali kubwa za Ulaya. Maana yake kama Samatta ataendelea kufanya vizuri, kuna nafasi ya kufanya kuuzwa pia. Kila la kheri kwake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni