pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 13 Januari 2017
Micho achekelea kupangwa na Tanzania Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda,Mulitin ‘Micho’ Sredojevic ameridhishwa na kupangwa kundi moja na timu za Tanzania na Cape Verde katika michuano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019. Lesotho ni nchi nyingine iliyopangwa katika kundi L. Akizungumza baada ya droo kutolewa, Micho, aliyefanikiwa kumaliza ukame wa Uganda kufuzu AFCON amesema Uganda wameangukia kwenye kundi stahili kabisa. ” Tunaweza kuhesabu droo hii kama ni nzuri, hii inathibitisha kazi nzuri tuliyofanya kwa miaka miwili hadi kupewa droo ya upendeleo. ” Micho amenukuliwa na mtandao wa Kawowo. ” Ni kundi linalochezeka, tunajua Cape Verde wanashuka kiwango, pia tunawafahamu ndugu zetu Tanzania. Comoro tuliochezea nao waliwabandua Lesotho. kiukweli wakati huu tutacheza na timu nyepesi . ” Mechi za kufuzu AFCON 2019 zimepangwa kuanza mwezi wa Sita huku Tanzania ikianzia nyumbani dhidi ya Lesotho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni