Alhamisi, 12 Januari 2017

CHELSEA YAPATA RUHUSA YA KUPANUA UWANJA Halmashauri ya Hammersmith & Fulham imeipa ruhusa klabu ya Chelsea kufanya ujenzi wa kupanua uwanja wao wa Stamford Bridge. Kamati ya mipango na maendeleo ya halmashauri hiyo imetoa maamuzi hayo baada ya kufanya kikao kilichochukua muda wa saa tatu unusu usiku wa jana jumatano. Uwanja huo ambao kwa sasa unachukua watu 41,490 utatanuliwa ili kuingiza watu 60,000. Imeripotiwa kuwa kiasi cha Pauni milioni 500 ndicho kitatumika katika ujenzi huo. Ubunifu wa uwanja huo utasimamiwa na wasanifu wa Majengo kutoka uswiss Herzog & De Meuron ambao wamehusika na ujenzi wa uwanja Bird's Nest wa Beijng na Uwanja wa Bayern Munich Allianz Arena. Ujenzi huo unataraji utakamilika kabla ya msimu wa 2021-22.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni