pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 18 Januari 2017
Gurdiola awasifu wachezaji wake kwa kupigwa nne Ni heri kuambiwa ukweli unaouma ili ukujenge na uweze kubadilika ila uongo mtamu utakupotosha na kukupoteza.Sikia Pep Gurdiola alichowaambia wachezaji wake. Pep Gurdiola anaonekana sasa mambo ni magumu sana.Toka amekuja Uingereza amekuwa na matokeo magumu sana katika ligi hii tofauti na ilivyotarajiwa.Ameshaanza kutolewa mbio za ubingwa na hakuna mwenye uhakika kama atamaliza katika top four msimu huu.Wengi walichotarajia sio kinachomtokea. Pengine hii sijui ni kuwapa moyo au kudata,kwani Pep amewapongeza wachezaji wake.Gurdiola amewaambia wachezaji wake kwamba walicheza vizuri zidi ya Everton.Katika mchezo huo ambao Gurdiola anawasifu wachezaji wake,City walikula kipigo cha mbwa mwizi cha goli nne kwa sifuri ugenini zidi ya Everton. Hii iliwashtua wachezaji wa City na inaonekana labda anajaribu kuwajenga kisaikolojia.Timu imefungwa goli nne leo hii wanasifiwa kucheza vizuri.Haieleweki uzuri huo Gurdiola ameuchukulia kwa sura gani.City wana makosa mengi kiuchezaji haswa eneo lao la ulinzi kuanzia alipo Stones na golikipa wao Bravo wanafanya makosa kila siku.Haihitaji maarifa makubwa sana kuona kwamba City wana ulinzi mbovu sana kwa sasa.Claudio Bravo golikipa aliyepewa nafasi baada ya Gurdiola kumruhusu Joe Hart aondoke hadi sasa ameruhusu goli 14 katoka mechi 22. Wikiendi iliyopita tuliona magoli kwa namna ambayo huezi amini kuwa hawa ni Man City.Makinda wapya wa Everton Lookman na Tom Davies walionekana kutowaogopa kabisa City na walicheza kwa kujiamini mno.Timu pinzani zinazocheza na Man City zimekuwa haziwapi heshima Man City kwani sio Etihad sio ugenini timu pinzani za Man City zinajaribu kuwapa presha mabeki wa City wanaoonekana kukosa umakini. Pep Gurdiola anaonekana wazi anastahili zigo la lawama kwa kumuachia Hart aonfoke,lakini pia Stones aliyenunuliwa kwa £50m anaonekana kupwaya mno.Ni kipindi ambacho Gurdiola alipaswa awaambie ukweli wachezaji wake kuhusu uzembe wanaofanya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni