pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 9 Januari 2017
Baada ya kuifunga Yanga 4-0 huu ndio mpango wa Azam kuelekea nusu fainali Mapinduzi Cup2017 Baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya Yanga, kocha wa muda wa Azam Idd Cheche anasema kikosi chake kipo tayari kuikabili Taifa Jang’ombe. “Tunaamini Taifa Jang’ombe ni wazuri ni timu ambayo inajilinda sana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa hiyo mbinu ambayo tutaitumia tutajua tunafanyaje hatuwezi kusema mapema,” anasema Idd Cheche kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Taifa Jang’ombe. “Mechi ya kesho ni tofauti na mechi iliyopita, mechi iliyopita imeshapita lakini mechi ya kesho tunaiangalia kwa namna yake kutokana na timu ya Taifa Jang’ombe ilivyo na sisi tunajipanga ni jinsi gani ya kukukabiliana nao.” “Hilo suala bado ni nyeti kwa sababu unapoenda kupambana na mpinzani wako, unaangalia uzuri wa mpinzani wako na wachezaji wako kwa sababu wachezaji wanatofautiana kila mtu ana uwezo wake, sasa unaangalia mchezaji gani anaweza kukusaidia kutokana na mchezo wenyewe basi ndio unamtumia.” Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2017 (Azam FC vs Taifa Jang’ombe utachezwa saa 10:15 jioni kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni