pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 15 Januari 2017
AFCON: Hii itakua hatari sana Senegal Vs Tunisia leo.Moja kati ya mechi bora katika hatua hizi za makundi ni mechi kati ya Senegal Vs Tunisia ambayo inafanyika leo kwa kukutanisha timu mbili zenye talent kubwa. Tunisia inaongozwa na kocha Henri Kasperczak ambae ametengeneza ukuta wa kuaminika kwenye kikosi hicho cha Tunisia. Imekua ni ngumu kupasua ukuta wa Tunisia ambapo wameruhusu magoli 3 tu kwenye mechi 6 na walimaliza namba moja kwenye group lao la qualifying. Hii ni moja kazi kubwa ambayo Henri Kasperczak anasifika kwenye kikosi cha sasa cha Tunisia. Ukija kwa Senegal wanasifika kwa kuwa na safu hatari ya ushambuliaji. Pia ukizingatia wanatajwa kuwa ni timu bora kwa sasa kwa bara la Africa kwa kuzingatia vitu vingi kwenye kikosi kizima. Sadio Mane ametoka kwenye perfomance nzuri kwenye ligi ya EPL na anategemewa kufanya maajabu kwenye michuano hii kama alivyoanza Aubemanyang wa Gabon. Mchezaji wa Valencia Aymen Abdennor ndie mtu wakutegemewa zaidi kwenye ulinzi wa Tunisia. Tough defender anategemewa kuongoza safu hiyo ili kumuweka salama golikipa legend Aymen Mathlouthi. Kutoka kwenye mechi zao tano zilizopita kwa upande wa Tunisia ni L D W W W na Senegal ni W D L W W. Wachezaji mashuhuri wa kuwaangalia kwernyr mechi hii ni Aymen Abdennour na Aymen Mathlouti wote wa Tunisia. Sadio Mane na Cheikhou Kouyate wa Senegal. Mechi hii kama kawaida watanzania wote wataangalia kwenye kituo cha kitanzania kilichopewa nafasi ya kuonyesha michuano hii ZBC 2. Kwa njia rahisi ZBC 2 wanapatikana kwenye king’amuzi cha Azam Tv channel namba 116.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni