Ijumaa, 13 Januari 2017

Mayanja amekubali yaishe… Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amekubaliana na matokeo ya kufungwa na Azam kwenye mechi ya fainali ya ya Mapinduzi Cup, amesema imekuwa kama bahati mbaya tu timu yake kupoteza mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam. Kocha huyo raia wa Uganda amesema, kiufundi Simba iliupiga mwingi mno lakini imekuwa kama bahati mbaya kupoteza mechi hiyo. “Sisi tumecheza kitimu, tumecheza mpira mwingi sana kwa hiyo imekuwa kama bahati mbaya,” anasema Mayanja baada ya Simba kulazwa kwa bao 1-0 na Azam FC. “Niwapongeze Azam kwa kushinda ubingwa wa Mapinduzi, walipata nafasi moja wakaitumia vizuri wakapata ushindi.” “Sasa tunaenda kufanya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni