Jumapili, 15 Januari 2017

SENEGAL YA KWANZA KUSHINDA AFCON 2017, YAILAZA TUNISIA 2-0 SENEGAL imekuwa timu ya kwanza kushinda mechi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu, baada ya kuilaza Tunisia 2-0 katika mchezo wa Kundi mjini Franceville usiku wa Jumapili. Baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo kati ya Zimbabwe na Algeria, Simba wa Teranga sasa wanaongoza Kundi hilo kutokana na ushindi wao uliotokana na mabao ya Sadio Mane dakika ya 10 kwa penalti na Kara Mbodj dakika ya 30. Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Senegal bao la kwanza Kikosi cha Senegal kilikuwa: Abdoulaye Diallo, Kara Mbodj, Cheikh M'Bengue, Lamine Gassama, Cheikhou Kouyate/Papakouli Diop dk88, Kalidou Koulibaly, Sadio Mane, Keita Baldé Diao/Ismaila Sarr dk62, Idrissa Gueye, Pape Alioune Ndiaye/Henri Saivet dk72 na Mame Biram Diouf. Tunisia: Aymen Mathlouthi, Hamdi Nagguez, Ali Maaloul, Aymen Abdennour, Syam Ben Youssef, Larry Azouni/Wahbi Khazri dk46, Naim Sliti, Youssef Msakni, Ferjani Sassi, Hamza Lahmar na Ahmed Akaichi/Taha Yassine Khenissi dk64. Mapema katika mchezo uliotanguliwa wa kundi hilo, Algeria na Zimbabwe ziligawana pointi kwa sare ya 2-2. Mabao ya Algeria yalifungwa na Mwanasoka Bora Afrika, Riyad Mahrez yote dakika za 12 na 82, wakati ya Zimbabwe yalifungwa na Kudakwashe Mahachi dakika ya 17 na Nyasha Mushekwi kwa penalti dakika ya 28. Algeria: M’Bolhi; Belkhither/Meftah dk46, Mandi, Bensebaini, Ghoulam; Guedioura, Bentaleb; Mahrez, Brahimi, Soudani/Ghezzal dk77 na Slimani. Zimbabwe: Mkuruva; Nhamoinesu, Zvirekwi, Muroiwa, Bhasera; Phiri, Mahachi, Katsande, Billiat, Mushekwi/Malajila dk78 na Musona/Rusike dk11. MIchuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi C, mabingwa watetezi Ivory Coast wakimenyana na Togo ya beki wa Yanga, Vincent Bossou na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Morocco usiku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni