Jumanne, 17 Januari 2017

Asante Van Gaal…utamkumbuka kwa lipi? Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.Hivyo ndivyo niwezavyo kusema. Pengine labda ni taarifa ambayo wanasoka wengi hawakuitaraji kuisikia ila yametimia.Baada ya kukaa kwenye soka kwa muda mrefu hatimae Louis Van Gaal ameamua kustaafu soka.Watu wengi tulitaraji labda ataonekana tena viwanjani siku za karibuni.Wengi walihisi huenda atakuwa kocha mpya wa PSG lakini majukumu ya familia ni muhimu zaidi kwake,kaamua kuilea familia. Pamoja na kupokea ofa kubwa kutoka klabu moja ya Asia ya £ 44 kwa misimu ya miaka mitatu,l akini Van Gaal ameikataa ofa hiyo na ameamua kuachana na soka akiwa na miaka 65. Sababu za Van Gaal kustaafu soka ghafla hivi inasemekana ni kutokana na matatizo ndani ya familia yake. Van Gaal ameamua kustaafu ili kuwa karibu na familia yake. Haswa kuwa karibu na binti yake ambaye alimpoteza mumewe siku za karibuni. Katika Interview aliyofanyiwa Van Gaal alisema “nadhani ni muda umefika,nilitaka kufanya hivi baada ya kombe la dunia lakini nikaenda Manchester,nilidhani tena nitaacha ila sikuacha lakini sasa ni wakati ambao sidhani kama nitakuwa kocha tena” Van Gaal ni kati ya makocha wenye rekodi katika soka kwani ameshawahi kuwa kocha wa Ajax,Barcelona,Bayern Munich Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi.Lakini pia akiwahi kuzichezea Ajax,Az,Sparta Rotterdam,Telstar na Royal Antwerp.Van Gaal baada ya kuiongoza Uholanzi katika mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 alijiunga na Manchester United lakini hakuwa na msimu mzuri na ilipofika 2016 Manchester United walikatisha mkataba wao na Mholanzi huyu lakini akiiachia Manchester United ubingwa wa FA. Van Gaal alianza kuwa kocha rasmi mwaka 1991 akiifundisha Ajax akiisaidia kuchukua makombe matatu kwenye ligi 1994,1995 na 1996 huku msimu wa mwaka 1995 akiwa hajafungwa kwenye ligi ya nyumbani na UEFA. Akiipa pia Ajax kombe la UEFA mwaka 1995. Baada ya kuondoka Ajax alienda Nou Camp kuifundisha Barcelona.Akiwa huko alikumbana na upinzani kutoka vyombo vya habari na hata wachezaji kutokana na tabia yake ya kubadilsha namba wachezaji.Mfano halisi ni pale alipotaka acheze pembeni kama winga lakini Rivaldo akitaka kusimama katikati.Lakini akawasaidia kubeba La Liga mwaka 1998 na 1999. Mwaka 2000 alirudi kuifundisha timu ya taifa ya Uholanzi.Aliporudi Uholanzi ilikuwa majanga kwani Van Gaal alishindwa kuipeleka timu kombe la dunia hiyo ikiwa mara ya kwanza toka1986. Mwaka 2002 alibwaga manyanga Uholanzi na kurudi Barcelona.Akionekana kuandamwa na pepo mbaya Van Gaal akiwa Barcelona matokeo yalikuwa mabovu sana kwani aliiacha timu ikiwa nafasi ya 12 akatimuliwa. Alirudi nyumbani Ajax mwaka 2004 lakini akaingia kwenye mgogoro na kocha mkuu wa Ajax Ronald Koeman ambae sasa yuko Everton akahamia Az ya kwao Uholanzi lakini nako akaiacha na kwenda Bayern Munich mwaka 2009 na kumsaini Arjen Roben toka Real Madrid.Van Gaal akiwa Bayern alionekana kuwaamini sana vijana wadogo kama Muller na Badstuber na mwaka 2010 akiwapa kombe la Bundesliga lakimi mwezi March mwaka 2011 Bayern walikatisha mkataba wake. 2012 alirudi timu ya taifa ya Uholanzi na kuisaidia kuingia kombe la dunia.Wakati wa mashindano hayo Van Gaal na mfumo wake wa 3-5-2 waliiporomoshea kipigo timu ya taifa ya Hispania cha magoli matano. Lakini wakaondolewa na Argentina katika hatua ya nusu fainali.Baada ya Uholanzi kutolewa kocha Van Gaal aliitwa OT kurithi mikoba ya Davies Moyes ambako hakuwa na mdimu mzuri achilia mbali kombe la FA alilowapa. Huyo ndio Van Gaal ambae kwa sasa anaona ni heri uzee wake akae na wanae kuliko kuendelea na soka.Mchezaji wa zamani wa Uholanzi alilitabiri hili kwani alishawahi kusema kwa kilichomtokea Van Gal Manchester anahisi atastaafu soka na kuanza kuwa mtazamaji wa soka,utabiri wa And De Boer unaonekana kukamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni