pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 12 Januari 2017
YANGA WAIFUATA MAJIMAJI JUMANNE SONGEA Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM VIGOGO wa soka, Azamm Simba na Yanga watarejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katikati ya mwezi huu baada ya mapumziko ya tangu mwishoni mwa mwaka kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi. Yanga iliyoishia katika Nusu Fainali baada ya kutolewa na Simba SC Jumanne kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar yenyewe itacheza Jumanne ya Januari 17, mwaka huu. Yanga watakuwa wageni wa Maji Maji Jumanne ya Januari 17, mwaka huu Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Siku hiyo, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu watakuwa wageni wa Majimaji Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma katika mfululizo wa Ligi Kuu, wakati Simba inayokutana na Azam katika fainali ya Kombe la Mapinduzi kesho zitarejea siku inayofuata Ligi Kuu. Simna watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar Jumatano ya Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wakati Azam watakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala mjini Dar es Salaam. Mchezo huu wa Azam na Mbeya City utaanza Saa 1.00 usiku wakati michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni