Ijumaa, 13 Januari 2017

Simba, Yanga, asanteni kwa kuja Zanzibar Hatimaye timu ya Azam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taji la Mapinduzi baada ya ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Bao safi la Himidi Mao akipasia nyavu kwa shuti kali akiwa nje ya box ndilo limeipa Azam kwa mara ya tatu wa kombe hilo. Awali timu za Simba na Yanga zilipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na moto wao kwenye ligi kuu Tanzania bara huku Azam ikipewa nafasi ndogo kwa kuangalia rekodi zake kwenye ligi pamoja na kuondokewa na kocha wao siku za usoni. Rekodi za Azam bada ya kuchukua ubingwa wa Mapinduzi 2017 Azam ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu goli hata moja kwenye mashindano ya mwaka 2017. Ubingwa wa mwaka 2017 unaifanya Azam kuifikisha mataji matatu na Simba kwa idadi mataji ya Mapinduzi tangu mwa 2007. Azam imechukua taji hilo mwaka 2012, 2013 na 2017. Azam imezifunga Simba na Yanga kabla ya kutwaa taji la Mapinduzi 2017 (Azam 4-0 Yanga mechi ya nusu fainali, Azam 1-0 Simba mchezo wa fainali)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni