pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 18 Januari 2017
LIVE KUTOKA JAMHURI: MTIBWA SUGAR 0 VS 0 SIMBA (FLL TIME) MPIRA UMEKWISHAAA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 89, Mtibwa wanafanya kazi ziada kuokoa mpira wa faulo Dk 86, Kipa Mohammed anafanya kazi ya ziada na kuugusa mpira uliokuwa unajaa wavuni, kona. Simba wanachonga lakini haina madhara SUB 85, Mtibwa Sugar wanamuingiza Hussein Javu kuchukua nafasi ya Jaffar Salum SUB Dk 83 Simba wanamtoa Kichuya, nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate Dk 81, nafasi nzuri kwa Mtibwa, mabeki wa Simba wanagongana na mpira unamkuta Friday, lakini anapinga shuti matege....hakuna kitu Dk 79, Mandawa tena, anaachia mkwaju mkali lakini anapaisha juuu SUB Dk 77, Barnabas anaingia Kelvin Friday SUB Dk 75, Simba wanamtoa Kazimoto na nafasi yake inachukuliwa na Pastroy Athanas Dk 73, Ajibu anafanya kazi ya kugeuka na kuachia shuti hapa, Said Mohammed anaokoa na kuwa kona ambayo haina madhara Dk 72, Mandawa amegeuka anapiga shuti kali kabisa hapa lakini Agyei anadaka kwa ufundi mkubwa kabisa Dk 70, Banda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini unamgnga beki Mtibwa na kuwa kona Dk 68, Kichuya anawachambua mabeki wa Mtibwa lakini Shomari anatoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa Dk 65 Baba Ubaya anagongana na Hamad Juma na wote wako chini wanatibiwa KADI Dk 64, Issa Rashid "Baba Ubaya" analambwa kadi yah njano kwa kumuangusha Kazimoto Dk 59, Kichuya anamtoka Baba Ubaya, krosi safi kabisa lakini Mbonde anaruka na kupiga kichwa safi kabisa Dk 57, Liuzio anamzidi mbio Henry lakini anashindwa kuudhibiti mpira kutokana na uwanja kuwa mbovi Dk 54, Simba wanamuingiza Ajibu kuchukua nafasi ya Mavugo Dk 50, mpira bado unakuwa ni wa kubutua zaidi lakini safu ya ulinzi ya Simba wanapaswa kuwa makini hasa pembeni DK 45,Mtibwa wanaanza kwa kasi, krosi matata ya barnabas nakuwa kona MAPUMZIKO Dk 44, MAvungo anajaribu kuingia tena lakini Henry Joseph anaondosha hatari Dk 41 Mavugo anageuka na kuachia fataki hapa, linatoka kidogo juu la lango la Mtibwa Dk 37, Luizio na Kotei wanafanya kazi nzuri hapa, wanagongeana vizuri lakini shuti la Mavugo linashindwa kulenga Dk 36, ladha ya mpira ni butuabutua zaidi kuliko pasi za uhakika Dk 31 Kotei anafanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni mwa Chanongo akiwa anakaribia kuachia fataki karibu na lango la Simba. Inakuwa kona, inachongwa na Issa Rashid lakini Simba wanaokoa Dk 28, Luizio anamtoka Ali Shomari, anapiga krosi safi kwa Mavugo akiwa yeye na kipa Mohammed lakini anashindwa kufunga Dk 20, hakika mpira hauna mvuto sana. Mtibwa Sugar wanapata kona, inachongwa vizuri na Mandawa anapiga kichwa safi kabisa, lakini Agyei anadaka vizuriDk 15 Kotei mita 28 anaachia shuti kali lakini Said Mohammed anadaka vizuri kabisa Dk 14, Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi kali hapa, lakini Simba wanaokoa na kuwa kona. anaichonga Baba Ubaya lakini Simba wanaokoa vizuri Dk 11 sasa, mechi ina presha kubwa. Lakini zaidi mpira unachezwa katikati na uwanja unaendelea kuonekana tatizo katika umiliki wa mpira Dk 6, Simba wanapata kona, anaichonga hapa Kichuya lakini ni kona hovyoooo Dk 4 mpira safi wa krosi wa Hamad Juma lakini unakosa mtu, Mtibwa wanaokoa Dk 1, mpira umeanza lakini ikionekana kuanza kwa kubutua. Mtibwa wanapata faulo si mbali na lango la Simba KIKOSI MTIBWA: 1-Said Mohamed 2-Ally Shomary 3-Issa Rashid 4-Henry Joseph 5-Salim Mbonde 6-Shaban Nditi 7-Haruna Chanongo 8-Ally Makarani 9-Rashid Mandawa 10-Jaffary Salum 11-Vicent Barnabas SUB -Benedict Tinoko -Rogers Gabriel -Kassian Ponera -Dickson Daudi -Ibrahim Rajabu Jeba -Kelvin Friday -Hussen Javu KIKOSI SIMBA: 1. Daniel Agyei, 2. Hamad Juma, 3. Mohamed Zimbwe 4. Abdi Banda 5. Method Mwanjale, 6. Jonas Mkude 7. Shiza Kichuya 8. James Kotei 9. Laudit Mavugo 10 Juma Liuzio 11. Mwinyi Kazimoto Sub… Peter Manyika Novatus Lufunga Jamal Mnyate Pastory Athanas Mzamiru Yassin Ibrahim Ajibu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni