Jumatano, 11 Januari 2017

MESSI, NEYMAR, SUAREZ WAIPELEKA BARCA ROBO FAINALI Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akijaribu kumtoka Benat Etxebarria wa Athletic Bilbao katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Mfalme usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Barca ilishinda 3-1 mabao yake yakifungwa na Suarez dakika ya 35, Neymar kwa penalti dakika ya 48 na Messi dakika ya 78, huku la wageni likifungwa na Enric Saborit dakika ya 51 na Barca inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-3, baada ya awali kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza ugenini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni