Ijumaa, 13 Januari 2017

LIVE KUTOKA KWENYE UWANJA WA AMAAN, FAINALI YA MAPINDUZI; AZAM FC 1 VS 0 SIMBA SUB Dk 42, Simba wanamtoa Kazimoto na nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo raia wa Burundi Dk 40, krosi safi ya kazimoto, Manula anapangua na mpira unamkuta Kichuya katika nafasi nzuri lakini anashindwa kufunga Dk 36 sasa, mpira unachezwa zaidi katikati ingawa Simba wanaonekana na presha ya kutaka kusawazisha hilo bao KADI Dk 33, Sure Boy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kotei lakini anamlaumu mwamuzi kwa kupuliza filimbi Dk 32, Simba wanagongeana vizuri hapa na Kichuya anaachia shuti kali lakini hajalenga lango Dk 30, Simba wanaonekana kucheza zaidi na kusukuma mashambulizi mengi kwenye lango la Azam FC Dk 28, Banda anaachia shuti kali la mkwaju wa adhabu lakini Manula anaonyesha umahiri wa juu anapangua na kuwa kona, inachongwa na wachezaji Azam FC wanaokoa Dk 26, Krosi nyingine ya Zimbwe, Yakubu anaruka na kupiga kichwa, konaaa, inachongwa na Kotei lakini Azam wanaokoa. Dk 25, Simba wanagongeana vizuri na Bukungu anatumbukiza krosi safi hapa lakini Mohammed anaokoa vizuri kabisa Dk 21 sasa, kidogo unaonekana kama Azam FC wanapunguza kasi ya mchezo huku Simba wakifanya kila linalowezekana kutaka kupata bao Dk 19, Kotei anachia fataki maridadi hapa, lakini mpira unapita juu ya lango la Azam Dk 18, Simba wanafanya shambulizi tena lakini krosi ya Bukungu inaishia mikononi mwa Manula Dk 15, Azam FC wanafanya shambulizi jingine, Bocco anaachia fataki lakini hakulenga lango GOOOOOOOOO Dk 13, Azam FC wanaandika bao safi kabisa, Himid Mao anaachia fataki hapa linalomshinda Agyei na kujaa nyavu za juu Dk 10, Azam FC wanafika kwenye lango la Simba, lakini Yahaya anaachia shuti kuuubwaaaaa Dk 9, Simba wanaingia vizuri, Kotei anazuiwa na Mkude anaachia shuti kuuubwa juu Dk 5 sasa, mpira unaonekana kutokuwa na kasi sana, huenda ni uoga kutoka kwa kila timu kuhofia kuruhu bao la mapema Dk 2, Kichuya anatimua mbio kutoka katikati ya uwanja lakini Azam FC wanakuwa makini na kuondosha hatari ndani ya 18 Dk 1 mechi imeanza taratibu huku kila timu ikionekana kujipanga vizuri tena kwa umakini mkubwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni