pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 13 Januari 2017
Ripoti kutoka Gabon: Wananchi wagomea AFCON ikiwa yamebaki masaa machache. Na mwandishi wetu kutoka Gabon naona maandalizi ya AFCON yamekamilika kwenye ngazi zote hadi Rais wa hapa anahusika kwa kiasi kikubwa sana. Lakini baadhi ya wanaonchi wanagoma kuhusu uwezo wa Gabon kuweza kuandaa mashindano haya. Wananchi wanadai kwamba nchi yao ina matatizo mengi ya kiuchumi na kijamii zaidi ya kutumia pesa kujiandaa na mashindano hayo. Mwananchi mmoja alisema,“AFCON sio kitu kibaya lakini kwa sisi raia wa Gabon hatuko tayari kuandaa haya mashindano. Tuna matatizo mengi sana kwa mfano angalia tu nyumba zilizopo pembeni ya viwanja, zinaonyesha kabisa dalili ya hali mbaya. Kuna watu hawana makazi wanaishi nje ya uwanja. Bora hizi pesa na attention ingetumika kumaliza angalau matatizo haya” Sio watu wote wanaopinga AFCON kufanyika Gabon, baadhi yao wanasema ni wakati muafuka. “Mimi napinga swala la wananchi kupinga na kuandamana kuhusu AFCON, tukio hili linawaleta watu pamoja, linawaunganisha. Ni muhimu sana kuuangana kupitia michezo. Hatuwezi kuacha AFCON isitokee hapa kwetu Gabon”. Gabon inasifika kwa kuwa mmoja kati ya nchi zinazozalisha mafuta lakini takwimu za benki ya dunia zinaonyesha kwamba theluthi ya wananchi wake wanaishi kwenye hali mbaya ya umaskini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni