Alhamisi, 12 Januari 2017

Alichokisema Mayanja kuhusu Azam kuelekea fainali ya Mapindu Cup2017 Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amewatoa shaka mashabiki wa mnyama kuhusiana na kasi ya Azam hususan baada ya mtani wao kuchezea kipondo cha maana. Mayanja amesema, mechi ya Azam na Simba ina tofauti yake ukizingatia utakuwa ni mchezo wa fainali. “Mechi ya Azam na Simba inatofauti yake, hiyo kasi ya Azam haiwezi kuja kesho kwa sababu fainali ni fainali,” anasema Mayanja wakati akizungumzia mchezo wa fainali ya Mapinduzi kesho Ijumaa, January 12, 2017. “Maandalizi yapo vizuri kabisa, Blagnon ndio anamajeraha lakini Mohamed Ibrahim yeye bado hana asilimia 100 za kucheza lakini wengine wote wako vizuri,” Azam imelichukua kombe la Mapinduzi mara mbili (2012 na 2015) tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo wakati Simba tangu 2007 wamelibeba mara tatu (2008, 2011 na 2015).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni