Ijumaa, 13 Januari 2017

Kuzifunga Simba na Yanga ni sawa na kukamata Kambale – Kocha Azam FC Baada yashinda kuiongoza Azam kushinda ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa kuifunga Simba 1-0 kwenye mechi ya fainali, kocha wa muda wa Azam FC Idd Cheche amesema, kuzifunga Simba na Yanga ni kama kumkamata Kambale (aina ya samaki). Cheche anasema hivyo baada ya kufanikiwa kuvifunga vilabu hivyo vikongwa vya kwenye soka la Tanzania na kupata matokeo kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua makocha wengi nchini pindi wakutanapo na vilabu hivyo. “Mshikamano na umoja wetu kwa sababu mimi timu zote nazijua, najua kila timu ipoje kwa hiyo ni kama vile unataka kumkamata Kambale, ukimshika kichwa basi hana ujanja,” anasema Cheche ambaye ameiongoza Azam katika mechi tano za Mapinduzi uku timu ikishinda mechi nne na kutoka suluhu mchezo mmoja. Cheche hakuacha kuwapongeza wapinzani wake wa mchezo wa fainali kwa kusisitiza kuwa licha ya Azam kuibuka na ushndi lakini mchezo haukua rahisi kwao. “Mchezo ulikuwa mgumu, nawapongeza Simba walijitahidi kutupa presha lakini mwisho wa siku tumeshinda.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni