pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 12 Januari 2017
Dawa ya Simba ipo tayari, bado kuwanywesha tu – Kocha Azam FC Baada ya mishemishe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kesho Ijumaa January 13 ndio kilele cha kombe la Mapinduzi michuano ya 11 ambayo ilizinduliwa rasmi December 30. Kuelekea mchezo wa huo utakaoshuhudia Azam na Simba zote zinazocheza ligi kuu Tanzania bara zikipambana, kocha wa muda wa Azam Idd Cheche amesema tayari anayo dawa ya Simba kilichobaki ni kuwanywesha. “Kila timu na dawa yake, Simba dawa yao ipo wasubiri kunyweshwa,” anasema kocha wa muda Idd Cheche aliyeifikisha Azam hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup 2017 bila timu yake kuruhusu goli. “Timu hizi mimi nazifahamu tangu nikiwa mchezaji, nimecheza nazo nikiwa mchezaji na sasa hivi ni mwalimu najua najua jinsi ya kuzikamata. Sisi tunazitaka timu zinazojiamini kwa sababu sisi tunajiamini zaidi yao.” Mfumo “Kuna plan mpya nakuja nayo mtaiona siwezi kuisema mapema lakini nitawashangaza watu uwanjani.” Maingizo ya wachezaji wapya “Hili bado ni la ndani kwanza, hatuwezi tukalisema hadharani kwa sababu hii ni sawa na vita kwa hiyo tunajipanga kimya-kimya wakija kustuka wanakuta shughuli inaendelea.” Majeruhi “Wachezaji wangu wote wako vizuri isipokuwa Hamisi Mcha ambaye ana matatizo kidogo.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni