Alhamisi, 19 Januari 2017

REAL MADRID SASA WAGEUKA VIBONDE, WAGONGWA TENA HISPANIA Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akimruka Gustavo Cabral wa Celta Vigo katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Mfalme usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Celta Vigo ilishinda 2-1 ugenini, hicho kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa Real Madrid kufuatia wiki iliyopita pia kufungwa 2-1 na Sevilla katika La Liga baada ya kucheza mechi 40 bila kufungwa. Bao la Real lilifungwa na Marcelo dakika ya 69 wakati ya Celta Vigo yalifungwa na Iago Aspas dakika ya 64 na Jonny Castro dakika ya 70 P

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni