Alhamisi, 12 Januari 2017

Lwandamina, Pluijm, hali tete Yanga Si kila tabasamu linamaanisha furaha au amani, ndivyo navyoweza kusema, ukiwaona machoni ni watu wenye sura zenye amani na furaha lakini mioyoni mwao wanajua wenyewe, hawa ni Hans van Pluijm na George Lwandamina. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimenifikia, Pluijm na Lwandamina hawana maelewano mazuri. Hali hiyo imesababisha kutokuwepo na utulivu kwa baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanadai Pluijm anasababisha makundi kwa wachezaji na kupelekea baadhi yao kutojituma kwenye timu. “Hans haelewani na Lwandamina, kuna ‘bifu’ zito kati ya wawili hao,” ni maneno ya jamaa aliyenitonya kuhusu hali ilivyo ndani ya Yanga yeye akiwa ni miongoni mwa viongozi wa kamati ya usajili ya usajili ya klabu hiyo. “Bifu hilo limepelekea uongozi wa Yanga kukaa kikao cha kutaka kumwondoa Pluijm lakini kuna baadhi ya viongozi bado wanamtaka Pluijm, lakini wapo ambao wanasema kwamba akiendelea watajiuzulu nafasi zao.” Tangu Lwandamina alipowasili ndani ya Yanga kama kocha mkuu, Hans van Pluijm alipewa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni